Recent News

KIST WACHEZA MPIRA WA MIGUU.

2023-11-13 08:17:05 category

Timu ya Mpira wa miguu ya Wafanyakazi kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), imewachapa vikali Timu ya Serikali ya Wanafunzi KISTSO.     

      Mchezo huo ulikuwa na upinzani mkubwa sana na kuleta matokeo ya 2:0, ambapo Timu ya   WAFANYAKAZI  WA TAASISI YA KARUME  imepata ushindi wa magoli 2 na Timu ya SEREKALI YA WANAFUNZI KISTSO imeangulia 0.

      lengo la Mchezo huo  ni kumuaga Mkufunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), ambae pia ni Mwalimu wa Michezo katika Taasisi ya Karume. Bw. Walid  Kassim Mohammed, ambaye anamaliza muda wake wa utumishi.

      Mchezo huo wa Mpira wa Miguu ulifanyika  katika Uwanja wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), uliopo Mbweni Zanzibar.