Recent News

KIST YAENDELEZA USHIRIKIANO NA GFP.

2023-11-13 08:24:02 category

Wawakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la uwekezaji rasilimali watu (GFP), linalojishuhulisha na masuala ya uchomeaji (Welding), Kutoka Nchini Marekani, wamefika katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Taasisi ya Karume, kwa kujadili mambo mbali mbali yenye lengo la kuendeleza ushirikiano katika elimu ya ufundi.

GFP inalengo la kuanzisha kituo cha umahiri wa uchomaji vyuma ili kuzalisha wataalamu wanaotambulika kitaifa na kimataifa katika nyanja ya uchomeaji vyuma (Certified Welding Engineer).