Recent News

KIST IMESHIRIKI WARSHA PAMOJA NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU.

2024-03-18 13:23:55 category

Wawakilishi kutoka Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar ikiwemo KIST, SUZA, ZU, na SUMAIT wakiwa katika Warsha ya siku moja ya kujadili namna ya kuifanya Zanzibar ya Kidigitali.

Kwa upande wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST), Naibu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Utafiti, Ubunifu na Ushauri Elekezi Dkt. Khamis Khalid Said aliwasilisha mada inayohusu Utambulisho wa Taasisi hiyo.

Warsha hiyo ilioandaliwa na Taasisi ya ONEWORLD imefanyika katika hoteli ya Jungle Paradise Resort iliopo Mbweni Zanzibar.